Waraka wa Baba Mtakatifu Frasisko juu ya hifadhi ya mazingira yetu Read more
ISBN 987-9966-60-052-3; pages 144: publication 2017
“LAUDATO SI,’ mi’ Signore” – “Utukuzwe ee Bwana
wangu.” Kwa maneno ya utenzi huu mzuri, Mtakatifu Fransisko wa Assisi
anatukumbusha kwamba mazingira yetu ni kama dada tunayeshirikishana maisha na
mama mzuri anayeinyoosha mikono yake ili kutukumbatia. “Utukuzwe ee Bwana wangu
kwa njia ya dada yetu, mama ardhi anayetudumisha na kutuongoza, na anayezaa
matunda mbalimbali yenye maua ya rangi na mimea.”
Dada huyu anatulilia kwa sababu ya athari
tulizomsababishia kwa kukosekana kwa uwajibikaji na matumizi yetu mabaya ya
rasilimali tulizojaliwa na Mungu. Tumefikia hatua ya kujiona kuwa sisi ndio
watawala wake, na wenye haki ya kuzipora rasilimali hizo tupendavyo sis. Vurugu
zilizopo mioyoni mwetu iliyojeruhiwa na dhambi zinajidhihirisha katika dalili
za magonjwa yaliyomo ardhini, majini hewani na katika aina zote za mifumo ya
maisha.
Specifications | Descriptions |
---|---|