Christopher Mallia; ISBN 9966-21-889-0; Kilichapishwa mwaka 2003; Kurasa 60 Read more
Katika kijitabu hiki utagundua jinsi Wakristu wenye msimamo walivyokabili kifo chao wenyewe wakiwa na msaada wa sakramenti ya Mpako wa wagonjwa. Sakramenti hii asili yake inaanzia katika Agano Jipya, hivyo mimi ninaifunua na kuiweka wazi ili tuweze kuona bayana jinsi Mpako wa Wagonjwa unavyoanza moja kwa moja kutoka katika maisha ya Yesu na wakristu wa kwanza. Baadaye bila shaka nilimwagalia Yesu mwenyewe katika Injili. Nilijaribu kuchunguza kuona jinsi alivyozichukulia athari zake hasa kwa kukabiliana na taabu na mateso ya kibinadamu yaliyomzunguka. Nilijaribu kuelewa kwa namna gani alivyokabili mateso yake mwenyewe na kifo chake. Maisha pamoja na mateso yote ya kibinadamu yanayomalizika na kifo, kwa hakika ni fumbo. Inamchukua Mtu-Mungu, kama Yesu kutoa jibu linalostahili kuhusu fumbo kama hili. Kijitabu hiki ni sehemu ya jibu hili. (kutoka kwenye utangulizi wa mwandishi)
Specifications | Descriptions |
---|---|