Christopher Mallia; ISBN 9966-21-893-9; Kilichapishwa mwaka 2003; Kurasa 64 Read more
Sakramenti ya Kipaimara ni nini? Je, sakramenti hii ina maana gani na ni upya wa namna gani unaotolewa na sakramenti hii kwa maisha ya mtu ambaye amekwisha pata ubatizo? Kwa namna ambayo tohara humfanya anayehusika kuwa mtu mzima na mshiriki kamili wa kabila, vivyo hivyo Sakramenti ya Kipaimara humwimarisha mtu kuwa Mkristo mwenye wajibu, akijihusisha kikamilifu kwenye maisha ya kanisa.
Kitabu hiki ni matokeo ya juhudi ya mwandishi kuwasaidia watoto na vijana waweze kujiandaa kwa tukio la kipekee la Kipaimara. Kitabu hiki kimegawanyika katika sehemu mbili: sehemu ya kwanza ni ufupisho kamili wa mafundisho ya Kipaimara na sehemu ya pili hutoa muhtasari wa mwitikio kutoka kwa vikundi ambavyo mwandishi amevifanyia maandalizi kwa ajili ya Sakramenti ya Kipaimara. Kitabu hiki kitakuwa cha manufaa sana kwa mtu yeyote anayewaandaa wengine kwa ajili ya Sakramenti ya Kipaimara pamoja na wale wote wanaokusudia kuimarisha maarifa yao kuhusu Sakramenti hii.
Specifications | Descriptions |
---|---|