ISBN 9966-60-285-5; Year of Publication 2023; Pages Read more
Kwa Maadhimisho ya Misa na Liturujia ya Vipindi Kadiri ya Kalenda ya Jumla ya Kiroma
Kwa vipindi mbalimbali vya siku, liturujia ya vipindi hueneza sifa na
shukrani, kumbukumbu ya mafumbo ya wokovu, sala na kionjo cha utukufu wa
mbinguni unaopatikana katika fumbo la Ekaristi, “Kitovu na kilele cha maisha
yote ya jumuiya ya kikristo.” Liturujia ya Vipindi vilevile ni maandalizi bora
kwa ajili ya adhimisho la Ekaristi yenyewe, kwa kuwa inahamasisha na kuimarisha
kwa njia ifaayo, mielekeo muhimu kwa ajili ya adhimisho kamilifu la Ekaristi:
iman, matumaini, upendo, ibada na roho ya kujikatalia. Utakaso wetu unatimia na
ibada inatolewa kwa Mungu katika liturujia ya vipindi kwa namna ambayo
mazungumzano yanaanzishwa kati ya Mungu na sisi, ambapo ‘Mungu anasema na watu
wake na watu wake wanamwitikia kwa nyimbo na sala.” Wale wanaoshiriki katika
liturujia ya vipindi wanaufikia utakatifu wenye utarajiri we pekee kwa njia ya
neon la Mungu linaoleta uzima, ambalo katika liturujia hii hupata msisitizo
mkubwa. Hivyo masomo yake hutoka katika Maandiko Matakatifu, maneno ya Mungu
katika zaburi yanaimbwa machoni pake, na maombi, sala, na nyimbo zikivuviwa na
Maandiko na kuinuliwa katika roho yake.
Specifications | Descriptions |
---|---|