ISBN 9966-08-281-6; Mwaka wa Kutolewa 2010; Idadi ya Kurasa 64 Read more
'Yesu na Familia yake' ni kitabu cha kwanza (1) katika mfululizo wa vitabu sita vya 'Safari ya Imani' vya mafundisho ya Katekisimu Katoliki. Kitabu hiki kimejikita hasa katika kufafanua mafundisho yahusuyo, Historia ya wokovu na Maandiko matakatifu. Kinafafanua maswali mbalimbali kama vile; Tuliipataje Biblia? Mungu amejifunua kwetu kwa namna gani? Kuwa hai kuna maanisha nini? Mfululizo wa vitabu vya katekisimu vya 'Safari ya Imani' vinatoa mwongozo kwa wakatekumeni wanaojitayarisha kupokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu, Kitubio, au Kipaimara kwa mara ya kwanza. Vitabu hivi pia vinaweza kuwasaidia wakristo kuimarisha imani yao na kuishi kwa furaha kama wafuasi wa Kristo, na kuwa mashuhuda wa kweli katika jamii yetu ya kisasa.
Specifications | Descriptions |
---|---|