Ua La Upendo

In Stock
$5.00

Na Fr John Joseph, vielelezo na S. Bullen; ISBN 9966-21-880-7; kurasa 40; kilichapishwa 2003: toleo la kwanza 2014 Read more

Tags: Ua, La, Upendo
Weight: 375 g
SKU: #8ycgmDeJOU

Kitabu hiki ni tafsiri ya maandishi ya maisha ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu aliyoyaandika yeye mwenyewe. Teresa wa Mtoto Yesu na wa Uso Mtakatifu, ni jina la kitawa la Thérèse Françoise Marie Martin, maarufu pia kama Teresa wa Lisieux, anayeheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mwenye sifa za bikira na mwalimu wa Kanisa. Kisha kujiunga na monasteri ya Wakarmeli Peku ya Lisieux akiwa msichana mdogo tu, usafi na unyofu wa maisha yake vilimfanya mwalimu wa utakatifu katika Kristo, akafundisha njia ya utoto wa kiroho ili kufikia ukamilifu wa Kikristo, akafanya kila juhudi ya kifumbo kwa ajili ya kuokoa watu na kustawisha Kanisa. Akifurahia udogo wake, Teresa alijitokeza kama “mtaalamu wa elimu ya upendo” (Papa Yohane Paulo II), katika maandishi yake, hasa katika shajara alimosimulia kwa unyofu wa hali ya juu jinsi kwa neema alivyoelewa na kutekeleza Injili katika maisha yake yaliyofichika monasterini. Alifariki akiwa na umri wa miaka 25 tu. Tangu mwaka 1927 ni msimamizi wa wamisionari wote (pamoja na Mt. Fransisko Saveri) na tangu mwaka 1944 ni msimamizi wa Ufaransa (pamoja na Yoana wa Arc). Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 1 Oktoba.

Specifications Descriptions

Latest Reviews

No Review
0

You May Also Like