Na Sr. Praxides Walumbe; ISBN 9966-08-545-9; Kilichapishwa Mwaka 2010; Idadi ya Kurasa 32 Read more
Kabla ya kupaa mbinguni, Yesu aliwapa maagizo ya mwisho mitume wake. Aliwaamuru kuwa wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba. "Yaani Yohane alibatiza kwa maji, bali ninyi matabatizwa kwa Roho Mtakatifu baada ya siku si nyingi" (Matendo 1:5). Mitume waliendelea kusali pamoja toka hapo Yesu alipopaa mbinguni mpaka siku ya Pentekoste. Na baada ya siku tisa, Roho Mtakatifu aliwashukia na hapo ndipo Roho Mtakatifu aliunda familia mpya yaani Kanisa. Siku hizi tisa za kusali zinaitwa 'Novena'. Na kila mwaka kipindi hiki cha Pasaka wakristo wakifuata nyayo za mitume, wanasali siku tisa kabla ya siku kuu ya Pentekoste.
Specifications | Descriptions |
---|---|