Maria Mama Yetu

In Stock
$1.00

Kimetafsiriwa na Padre John Kulwa, Segerea Seminary; ISBN 9966-08-952-7; Kilichapishwa Mwaka 2015; Idadi ya Kurasa 32 Read more

Tags: Maria, Mama, Yetu
Weight: 45 g
SKU: #bPhPT9M1r2

Mpendwa msomaji na mwana mpendwa wa Maria, mkononi mwako ni kijitabu ambacho kinakuingiza katika Novena kupitia Maria chini ya kichwa "Maria Mfungua Mafundo". Mama yetu Mfungua mafundo ni ibada ya hivi karibuni iliyoanza kwenye miaka ya 1984. Kardinali George Mario Bergolio, Askofu Mkuu wa Buenos Aires, ambaye leo hii ni Hayati Baba Mtakatifu Francis I aliingiza Argentina kadi hii takatifu na ilianza kufanya mizunguko katika miji mbalimbali. Idadi ya wanachama ilikuwa ikiongezeka na kila mmoja alitaka kuwa na picha hiyo na sala ambazo kwa njia yake walikuwa wakipata neema za pekee.

Katika maisha tunapenda, kutamani na kuhangaikia muungano wa ndani kabisa na Mungu na kila mmoja wetu. Tunajibidisha kufanya kazi kwa bidii sisi wenyewe lakini tunagundua kwamba hatuwezi kutoa jibu chanya kwa zawadi tupatayo bila mastahili yetu ya neema ambayo Mungu hutupatia. Je, inawezekana kukawa na mafundo yanayozuia makuzi yetu ya kiroho? Kuna mafundo ambayo hatuwezi kuyafungua sisi wenyewe isipokuwa kupitia msaidizi? Maria Mama yetu chini ya kichwa Maria Mfungua mafundo, amesimama mbele yako kwa sababu angependa kuwa sehemu ya safari yako ya kiroho hadi ufikie muungano wako na Mungu.

Specifications Descriptions

Latest Reviews

No Review
0

You May Also Like