Juu ya Upendo wa Kibinadamu na wa Kimungu

In Stock
$5.00

Waraka Rasmi Dilexit nos Kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko; ISBN 9966-60-362-3; Na. ya Kurasa 128; Mwaka wa Kutolewa: 2025. Read more

Waraka wa Papa Francisko Juu ya Upendo wa Kibinadamu na wa Kimungu unatoa mwaliko wa kugundua upya Moyo wa Yesu kama chemchemi ya upendo wa kimungu na kibinadamu unaoweza kuponya dunia iliyojeruhiwa. Katika nyakati za changamoto nyingi kama vile: kutawaliwa na mali na starehe, kupungua kwa thamani ya maisha ya kiroho, na mgawanyiko katika jamii, Papa anatuongoza “kurudi moyoni,” kugusa kiini cha utu na kuuona upendo wa Mungu unaoishi katika Kristo.

Katika sura kwa sura, anatuongoza:

·      Umuhimu wa Moyo kugundua utu wa ndani unaotutambulisha mbele za Mungu.

·      Matendo na Maneno ya Upendo kuona jinsi Yesu alivyoishi upendo wake kwa njia ya kukutana, kuponya na kusamehe.

·      Huu Ndio Moyo Uliopenda kwa Hali ya Juu teolojia ya ibada ya Moyo wa Yesu kama fumbo la upendo wa Mungu ulio wazi kwa wanadamu.

·      Upendo Unaotolewa kama Kinywaji Maandiko Matakatifu yakifunua upendo wa Mungu unaotiririka kwa ulimwengu ulio na kiu ya huruma.

·      Upendo kwa Upendo mwaliko wa kuishi upendo huo katika jamii, tukijitoa kwa waliojeruhiwa, maskini na waliotengwa.

 

Dilexit Nos ni mwanga mpya kwa ibada ya Moyo Mtakatifu wa Yesu si kama hadithi ya kihistoria, bali njia ya kuishi leo: upendo unaotutengeneza, kutuunganisha, na kutusukuma kwa jirani.

Ni waraka unaofaa kwa waamini binafsi, jumuiya za parokia, mashirika ya kitume, na yeyote anayetafuta uponyaji wa moyo na umoja wa familia ya Mungu.

Specifications Descriptions

Latest Reviews

No Review
0