Na Eugenia Campara, FSP; ISBN 9966-60-013-4; Kilichapishwa Mwaka 2016; Idadi ya Kurasa 40 Read more
Ujumbe wa Huruma ya Mungu si mpya katika mafundisho ya Kanisa. Katika maandiko matakatifu, Yesu mwenyewe anamdhihirisha Mungu kama Baba 'aliye mwingi wa huruma' (taz Ef 2:4). 'Huruma' kwa kweli ni moja ya mada kuu za utume wa Yesu Kristo. Inatosha tu kusoma mifano ya mwana mpotevu, msamaria mwema, mchungaji mwema, n.k, kuona kiwango cha upole wa Baba, usio na masharti na huruma kwa wanae, kama ilivyoonekana wazi. Tunaomba sala ya Huruma ya Mungu na novena ya Huruma ya Mungu, ambayo Yesu mwenyewe amemfunulia Mtakatifu Faustina, itusaidie kuimarisha imani yetu katika upendo wa Yesu mwenye huruma na kuonja, kwa njia yake, uzuri wa upendo wa Baba na huruma yake.
Specifications | Descriptions |
---|---|