Ufunuo wa Mungu unadhihirika bayana katika imani tamaduni na desturi za Waafrika. Methali na ngano za watu wa Afrika zinatuonyesha kuwa Roho Mtakatifu alipanda mbegu ya Habari Njema kwenye mila za Kiafrika hapo jadi, kabla ya watu wa Afrika kupata neno la Yesu na Mafunzo yake. Hadithi hizi kutoka Afrika zinasimulia mithali, masikitiko, ubadili, msamaha, neema, furaha, rehema, amani, mapatanisho, toba na umoja. Zinachunguza kwa undani uhusiano wa wanadamu katika yao wenyewe, na kati yao na Mungu. Hadithi hizi zinajitosa vilindini hata aina zinginezo za usemi na maandiko ya Kiafrika kama vile misemo, methali, sala, mashairi na nyimbo. Mwandishi amejumuisha pia matukio ya kweli katika maisha yake na wengineo barani, visa vinavyoleta upuzio, burudani na hata changamoto.
Specifications |
Descriptions |
|
|